PDF Archive

Easily share your PDF documents with your contacts, on the Web and Social Networks.

Share a file Manage my documents Convert Recover PDF Search Help ContactFADHILA ZA MWEZI WA MUHARRAM .pdf


Original filename: FADHILA ZA MWEZI WA MUHARRAM.pdf
Author: USER

This PDF 1.5 document has been generated by Microsoft® Word 2013, and has been sent on pdf-archive.com on 08/11/2015 at 22:29, from IP address 85.10.x.x. The current document download page has been viewed 620 times.
File size: 301 KB (3 pages).
Privacy: public file
Download original PDF file

Document preview


FADHILA ZA MWEZI WA MUHARRAM: { TAASUA’A -TAREHE 22/10, ‘AASHUURA-23/10/2015}
Alhamdulillaah, Tunamshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Kutufikisha tena katika mwaka
mwengine mpya wa Kiislamu. Katika mwezi wa Muharram, kuna fadhila zake maalumu juu ya kwamba
ni sawa na miezi mitukufu mingineyo. Fadhila nyingi Muislamu anaweza kuzipata atakapotekeleza
maamrisho ili aweze kujichumia thawabu nyingi. Mojawapo ni funga ya tarehe 9 na 10 Muharram
zinazojulikana kama Taasu'aa na 'Aashuraa. Hivyo ndugu Waislamu tusiache kufunga siku hizi mbili
kwani thawabu zake ni kama ilivyotajwa katika mapokezi yafuatayo:
‫ إني أحتسب على هللا أن يكفر السنة التي قبله)) رواه مسلم‬، ‫ (( صيام يوم عاشوراء‬: ‫قال النبي صلى هللا عليه وسلم‬
Kasema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Funga ya siku ya 'Aashuraa, nataraji kutoka
kwa Allaah Ayafute madhambi ya mwaka uliotangulia)) [Muslim]
(soma maelezo chini kujua kwanini tufunge pia na tarehe 9 Muharram)
Jumla ya miezi mitukufu ni minne na mwezi huu wa Muharram ndio mwezi wa kwanza unaoanza
kuhesabika kama ni mwaka mpya.
((Idadi ya miezi (ya mwaka mmoja) mbele ya Allaah ni miezi kumi na mbili katika ilimu ya Allaah
(Mwenyewe tangu) siku Alipoumba mbingu na ardhi. Katika hiyo imo minne iliyo mitukufu kabisa (nayo
ni Rajab, Dhul-Qa'adah, Dhul-Hijjah na Muharram) (kufanya) hivi ndiyo dini iliyo sawa. Basi msijidhulumu
nafsi zenu (kwa kufanya maasi) katika (miezi) hiyo)) [At-Tawbah 9:36]
Na Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema katika Hadiyth iliyotoka kwa Abu Bakr
(Radhiya Allaahu 'anhu):
Ni neema kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Kutujuaalia kuwa na miezi iliyo bora kuliko miezi
mingine au masiku bora au masaa bora kuliko mengine, ambazo thawabu za mema yanayotendeka
humo huwa ni zaidi ya nyakati nyingine.
Fadhila Za Mwezi Huu Khaswa
Ingawa miezi minne yote iliyotajwa katika Aayah ya juu ni mitukufu lakini mwezi huu wa Muharram
umefadhilishwa zaidi ya miezi mingine kama ilivyo katika Hadiyth zifuatazo:

‫صلهى ه‬
‫َعنْ أَبِي ه َُر ْي َر َة َرضِ َي ه‬
َ َ‫ص َي ِام َب ْع َد َر َمضَان‬
ََ ‫هللا ا ْل ُم َح هر ُم )) رواه مسلم‬
ِ ‫ش ْه ُر ه‬
ِ ‫سول ُ ه‬
ِّ ‫ضل ُ ال‬
َ ‫سلهم((أَ ْف‬
َ ‫هللا ُ َعلَ ْي ِه َو‬
َ ‫هللا‬
ُ ‫هللا ُ َع ْن ُه َقال َ َقال َ َر‬
Imepokelewa na Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kasema; Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi
wa sallam) amesema: ((Funga bora kabisa baada ya Ramadhaan ni funga ya mwezi wa Allaah wa
Muharram)) [Muslim]
Imepokelewa na Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma) ambaye amesema: "Sijapata kumuona Mtume
(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisubiri kufunga siku yoyote kama siku hii ya siku ya
'Aashuraa na mwezi huu yaani mwezi wa Ramadhaan" [Al-Bukhaariy]
Swawm ya 'Ashuraa imependezeshwa hata kwa watoto kuifunga kama walivyokuwa wakifanya
Maswahaba katika siku hiyo.

Kutoka kwa Ar-Rubay'i bint Mu'awwadh (Radhiya Allaahu 'anhaa) amesema: "Mtume (Swalla Allaahu
'alayhi wa aalihi wa sallam) alituma ujumbe Alfajiri ya siku ya 'Ashuraa katika vijiji vya Answaar
"Aliyeamka akiwa amefuturu amalize siku yake (kwa kutokula) na aliyeamka amefunga afunge" Akasema
(Ar-Rubay'i: 'Tulikuwa tukifunga baada yake na tukiwafungisha watoto wetu...' [Al-Bukhaariy na Muslim]

Sababu Ya Kufunga Siku Ya 'Aashuraa
Imepokelewa na Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma) kasema "Alielekea Mtume (Swalla Allaahu
'alayhi wa aalihi wa sallam) Madiynah akawaona Mayahudi wanafunga siku ya 'Aashuraa, akasema:
((Nini hii?)) (yaani kwa nini mnafunga?) Wakasema hii ni siku njema, hii ni siku Allaah Aliyowaokoa Wana
wa Israili kutokana na adui wao, na Muusa alifunga siku hii. Akasema (Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa
aalihi wa sallam): ((Mimi nina haki zaidi juu ya Muusa kuliko nyinyi)). Akafunga siku hiyo na akaamrisha
ifungwe" [Al-Bukhaariy]
Lakini Mtume wetu (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametufundisha kuwa tukhitilafiane na
Mayahudi kufunga siku hiyo kwa kuongeza siku moja kabla.
Imepokelewa na Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma) kasema "Alipofunga Mtume (Swalla Allahu
'alayhi wa aalihi wa sallam) siku ya 'Aashuraa na akaamrisha ifungwe wakasema: Ewe Mtume wa Allaah,
hii ni siku wanayoitukuza Mayahudi na Manaswara. Akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi
wa sallam): ((Ikifika mwakani In shaa Allaah tutafunga siku ya tisa pia)). Akasema (Ibn 'Abbaas) haukufika
mwaka uliofuata ila alifariki Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) [Muslim]
Kwa hiyo ni bora kufunga siku ya tisa na kumi Muharram, na kama mtu hakujaaliwa kufunga siku ya tisa
na kumi, basi afunge siku ya kumi peke yake ili asikose kupata fadhila ya siku hiyo.
Kwa vile siku hii ni siku Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Aliyomnusuru Muusa ('Alayhis-Salaam) na Wana
wa Israaiyli, na sisi pia tutakaofunga tuwe na tegemeo kuwa nasi Allaah (Subhaanahu wa
Ta'ala) Atatunusuru pia kutokana maadui wetu na mabaya kama Alivyotuahidi In shaa Allaah
((Bila ya shaka Sisi Tunawanasuru Mitume Yetu na wale walioamini katika maisha ya dunia ya siku
watakaposimama mashahidi (kushuhudia amali za viumbe)) [Ghaafir 40: 51]
Juu ya kwamba fadhila ya kufunga Swawm ni ibada Aipendayo kabisa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)
kama ilivyo katika Hadiyth mbali mbali, vilevile funga hii itatusafisha na madhambi ya mwaka mzima,
‫ إني أحتسب على هللا أنيكفر السنة التي قبله)) رواه مسلم‬، ‫ (( صيام يوم عاشوراء‬: ‫قال النبي صلى هللا عليه وسلم‬
Kasema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Funga ya siku ya 'Aashuraa, nataraji kutoka
kwa Allaah Ayafute madhambi ya mwaka wa nyuma)) [Muslim]
Ndugu Waislam, hii ni fursa kubwa ya kujisafisha na dhambi na kuzidisha taqwa (ucha Mungu) ili
kujibebea zawadi nyingi twende nazo Akhera kwa vile hatujui amali njema zipi zitakazokubaliwa na
Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) na hatujijui kama tutakuwa na umri wa kuchuma zaidi.

Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atujaalie katika wale ambao husikiliza kauli wakafuata zile
zilizo njema. Aamiyn.


FADHILA ZA MWEZI WA MUHARRAM.pdf - page 1/3
FADHILA ZA MWEZI WA MUHARRAM.pdf - page 2/3
FADHILA ZA MWEZI WA MUHARRAM.pdf - page 3/3

Related documents


fadhila za mwezi wa muharram
ramadaan shawwal 14 5
kayfa amalahoum en muslim
muongozo wa usalama kwa mujahidina
kitabu cha jihaad mashari al ashwaq
the murtadd vote


Related keywords
Copy tag