KUPOST KITAALAM KATIKA BLOG (PDF)
File information


Author: home

This PDF 1.5 document has been generated by Microsoft® Word 2010, and has been sent on pdf-archive.com on 21/08/2017 at 00:41, from IP address 196.249.x.x. The current document download page has been viewed 811 times.
File size: 4.41 MB (18 pages).
Privacy: public file
File preview


Hello Tanzania…!! Hi kwa ndugu na majirani wooote wa Madini Media…!!
Karibu tena ndani ya darasa la letu la msingi. Shukrani kwa Mungu katupa uhai na muda, basi leo
tuangazie swala zima la KUPOST KITAALAM KATIKA BLOG. Tutajifunza kupitia maandishi na
picha(sreenshot) ili kuweza kuelewa kwa undani zaidi kila hatua tunayofikia.
Naitwa Bin’Otto na utakuwa nami mwanzo hadi tamati ya somo hili. Na hii ni katika kutekeleza ahadi
ileee…, pale wengi mlipopenda post zangu na kuniuliza sana kuwa nawezaje kufanya vile, nikahaidi kuwa
kuna post inakuja yenye Madini hayo, au sio, ndiyo hii sasa, twende sawa.
Sitoweza kuongelea vyote ila tutagusa maeeo muhimu, ambayo ni pamoja na
1/ Kupost Article Yenye Maandishi
2/ Kupost Article Yenye Picha
3/ Kupost Article Yenye Link
4/ Kupost Article Yenye Audio
5/ Kupost Article Yenye Video.
Narudia tena, hapa tunasoma juu ya KUPOST tu, sio vinginevyo. Najua kuna wengi hawajajiunga na huu
mtandao lakini wanatamani sana, nipo kwa ajili yenu pia. Na masomo yote hata misaada inatolewa
bure, hivyo usiache kutusumbua kupitia coment au tuwasiliane kwa email, bonyeza hapa.
JINSI YA KUPOST ARTICLE YENYE MAANDISHI.
Hii ni rahisi kufanywa na yeyote yule anaejua kuandika baada tu ya kufungua article area (uwanja wa
kupost), na kwa sababu hiyo wengi hujitia ukichaa kwenye hii barabara ya lami ila nashangaa kwanini
huwa wanajikwaa sana na kuangukia ulimi wakati barabara walisema iko poa.
Sababu ni kwamba wao wanapost ilimradi, ila sisi tukapost kitaala ili tujitofautishe na wao. Na katika
eneo hili tutagusia post za aina mbili, yaani, ile ya kuanza kuandika moja kwa moja kwenye article area,
na nyingine, ni ile kukopy na kupest toka sehem moja kwenda kwenye article area.

1
Fiacrius K. Otto ©Madini Media (dakikazamadini.blogspot.com)

i.

Kutype moja kwa moja kwenye article area.

Okishafungua eneo la new post kuna vitu kadhaa vya msingi, kuwa navyo makini. Sehem ya kwanza
imeandikwa POST-TITLE, andika kichwa cha article yako katika sehemu hii. Inabeba idadi yeyote ya
maneno, hivyo niwewe kutambua ubora wa kichwa cha article unayoenda kuandika.
Kabla ya article area kuna ARTICLE-FORMATS, hii ndio sehem ya pili, si et ee. Anzia kushoto kuna neno
COMPOSE|HTML, basi we click compose. Ukiendelea utapata eneo la kuset FONT-TYPE/aina ya
mwandiko, FONT-SIZE/ukubwa wa maandishi, n.k yote yanaeleweka vizuri, tuendelee..
Na sehemu ya tatu ndio hiyo sasa, tunaita uwanja wa kujidai, ARTCLE-BODY. Hapo sasa unaruhusiwa
kuandika mambo yako yote. Na uwanja huu sidhani kama huwa unajaa, we fikiria hili somo limebeba
karibu topic sita lakini utashangaa, somo lote linaenea na inabaki sehemu ya uwanja wa mpira.
Baada ya hapo basi kuna jambo moja la muhim, upande wa kulia wa article body kuna kipengele cha
POST-SETTING. Na katika eneo hili cha msingi ni kuweka LABEL katika article yako mf HABARI, MAKALA,
nk, kutokana na wewe unataka habari yako iwe katika kipengele gani. Then Publish.

2
Fiacrius K. Otto ©Madini Media (dakikazamadini.blogspot.com)

ii.

Kukopy na kupest.

Hahaaa…!! Dah…!! Wabongo bhana, we acha tu. Wanyime chakula, poa, ila ukiwanyima kukopy na
kupest… hawatakusamehe…!! Anyway, hii huusisha kuchukua article mahara na kuihamishia kwako, na
hapa ndipo mabishoo wengi hujikwaa na kudharirika mbele ya watoto wadogo.
Ni lazima kufanya OPERATION kwanza ya ku-REMOVE ALL ARTICLE FORMATS kwenye mzigo ulioukopy
kabla ya kuupest katika blog yako. Sawa ee…!! Zipo njia nyingi ila kwa leo tutumie ya NOTE-PAD, ukitaka
nyingine labda unichek kupitia contact za mimi au Madini Media [Hapa]. Tuendelee.
Kopy mzigo wako fresh kutoka kwenye jasho la mwenzio, cha kwanza u-paste kwenye NOTE-PADE, then
click ENTER. Hapo utakuwa umeondoa format zote ikiwemo links na picha, na utakuwa umebaki na
maandishi tu. Then ya-kopy hapo kwenye NOTE-PAD na kuya-paste kwenye ARTICLE-BODY.
Dah kuna POST-TITLE tumesahau, mbona hujanikumbusha. Unaweza kuandika yako au ukai-CUT hapo
kwenye article body na kui-PASTE kwenye sehemu ya POST TITLE. Sawa ee, hapa kichwa ngum tu ndo
haelewi, ila wewe aaaaah we unaelewa vizuri tu. Unacheka…!! Omba sana usichemke…!!
Baada ya hapo unaweza badili mwandiko na format kadhaa ukaweka zako na watu wakajua kuwa wewe
ndo umeandika, kumbuka kuweka LABEL. Then Publish. Kwenye picha nilikopy toka kwenye article na
kupest kwangu, chek kwa makini hizo hatua nilizopita naamini utaelewa nilichokifanya.

3
Fiacrius K. Otto ©Madini Media (dakikazamadini.blogspot.com)

4
Fiacrius K. Otto ©Madini Media (dakikazamadini.blogspot.com)

Hapo sasa tumemaliza kipengele chetu cha kwanza, JINSI YA KUPOST ARTICLE YENYE MAANDISHI.somo
bado ni refu sana lakini ni tam kiukweli. Sema itakugharim sana kama huna hata kasoda pembeni basi
walau glasi ya juice, anyway, kama huna huna tu, heri ukae hivo kuliko kukopa.

5
Fiacrius K. Otto ©Madini Media (dakikazamadini.blogspot.com)

KUPOST ARTICLE YENYE PICHA
Zipo njia nyingi pia ila mimi nakupa hii kwanza nyingine utanichek labda maana dah, yapo mengi hapa ya
kuandika, nachoka. Nikwambie tu kwamba picha nilizozitumia hapo juu, ni screen-shot ya article
iliyokuwa na picha, hivo tufanye nasi kuweka ya kwetu ama ile ile, tutakavyoamua wenyewe.

Kwanza kabisa, PLACE CASER kwenye eneo unalotaka picha ikae. Kisha tembea hapo juu kwenye ICONS
mbalimbali, kuna kamoja ka mraba kenye rangi ya bahari kanajiita INSERT IMAGE. Click hapo utaambiwa
ADD-IMAGE, then utafuata maelekezo, ei, 1 upload, 2 choose file, 3 open, utaiona km hivi…

6
Fiacrius K. Otto ©Madini Media (dakikazamadini.blogspot.com)

Then ADD SELECTED, na hapo itahamia moja kwa moja kwenye uwanja wa post kwenye eneo uliloweka
caser. Click that image, utapewa wa maelezo mbalimbali kuhusu wapi unataka ikae vizuri, je ni kulia au
kusho au katikati, je kubwa au ndogo au original size, na pia kuna option ya kuandika CAPTION.

Mfano mimi naweza sema, picha yangu ikae upande wa kusoto/LEFT, isiwe kubwa wala ndogo yaani size
ya kati/MEDIUM. Then nikaamua kuitolea maelezo/CAPTION. Ehee kingine labda hiyo paragraph ya
kwanza nikaibold na kuipa rangi ya blue na ya pili nikaibold tu, then nika-jump break.

7
Fiacrius K. Otto ©Madini Media (dakikazamadini.blogspot.com)

Kabla huja-publish unaweza ku-preview ili uweze kuona itakavyokuwa ukipost, na ukiona iko sawa haina
haja ya kungoja wewe publish, na ukimaliza tuendelee na kipengele cha tatu. Dah sema natumia lugha
laini kama naongea vile yan, au nikasomee utangazaji… si et ee, nishauri basi, au acha.
KUPOST ARTICLE YENYE LINK
Ile ile post yetu kabla hatujai-pest kwenye note-pad na kubonyeza enter ilikuwa ina picha na links kibao. Sasa tayari
tumerudisha picha bado links. Mf ktk post hiyo kila ulipokutana neno MADINI MEDIA ndani yake ilikuwemo link hii
https://dakikazamadini.blogspot.com/ . sasa tuangazie njia kadhaa za kuirudisha hii link ktk post yetu.
i.

Kuweka link kwa uhalisia wake (viewed link)

Hapa unaweza kwenda katikaeneo ambalo unahitaji link yako ikae, ukaiandika kama ilivyo au ukaicopy mahari flani
ukaipest hapo kwako, na mtu akiibonyeza itampeleka kulekule ulikokusudia. Ubora wa hii njia ni kutambulisha
address kwa msomaji, ubovu wake ni pale address inapokuwa ndefu sana (utaonekana mshamba)

ii.

Kuweka neno lenye link ndani, (hidden link)

Unayehitaji kupost kitaalam hii ndio iwe njia yako sio hiyo hapo juu, okay?. Nenda hapo juu kwenye
icons mbalimbali, click LINK, utaona sehem mbili, ya juu andika neno mbadala ya link, na chini yake
andika au paste link address. Then click OK. Haitaonekana link bali lile tu NENO MBADALA.

8
Fiacrius K. Otto ©Madini Media (dakikazamadini.blogspot.com)

iii.

Kuweka picha yenye link ndani, (hidden link)

Hii mara nyingi inatumika kupost matangazo. Mf katika article hii naweza nikaamua katikati kuweka
picha ya tangazo, na ukiibonyeza hiyo picha inakupeleka kwenye ukurasa mwingine kabisa unaohusiana
na hilo tangazo. Na njia hii inatumiwa sana na bloggers kutokana na uhitajio flani.
Katika ile ile post yetu of course kuna picha nimeweka, ya mtu amepiga magoti kama anaomba. Hiyo
picha naweza kuiwekea link ndani yake, labda ya somo lenye title FAIDA ZA KUFUNGA NA KUOMBA,
then nikabadili caption nikaandika BONYEZA PICHA KUJUA MAOMBI YA KUFUNGA.
Njia inayotumika ni ile ile, HIDDEN LINK. Kule tuliweka link kwenywe neno hapa tunaweka link kwenye
picha. Click hiyo picha yako, click link, write a link address, click OK, umemaliza. Na ukibonyeza tu hiyo
picha itakupeleka moja kwa moja kwenye eneo la link uliyoiweka. Angalia hapa nachofanya

9
Fiacrius K. Otto ©Madini Media (dakikazamadini.blogspot.com)


Download KUPOST KITAALAM KATIKA BLOGKUPOST KITAALAM KATIKA BLOG.pdf (PDF, 4.41 MB)


Download PDFShare this file on social networks     

Link to this pagePermanent link

Use the permanent link to the download page to share your document on Facebook, Twitter, LinkedIn, or directly with a contact by e-Mail, Messenger, Whatsapp, Line..
Short link

Use the short link to share your document on Twitter or by text message (SMS)
HTML Code

Copy the following HTML code to share your document on a Website or Blog
QR Code to this page


QR Code link to PDF file KUPOST KITAALAM KATIKA BLOG.pdf


This file has been shared publicly by a user of PDF Archive.
Document ID: 0000653494.
Report illicit content